Mwanaharakati Mzalendo

‘JAMES BOND’ AANZA KUPONA, MOVIE KUTOKA 2020

Muigizaji Daniel Craig maarufu kama ‘James Bond’ amerejea mazoezini baada ya muda mrefu akiwa anauguza majeraha yake. 
Ukurasa rasmi wa Twitter wa movie ya James Bond umetoa taarifa kwamba muigizaji huyo ameanza mazoezi kufuatia kuumia kifundo cha mguu (Ankle) wakati wa kutengeneza filamu hiyo nchini Jamaica. 
Kuumia kwa Craig ni moja ya vikwazo vya kuchelewa kwa utengenezaji wa filamu hizo za Bond, ukiacha milipuko mitatu iliyotokea wakati wakitengeneza filamu hiyo kwenye moja ya jumba kubwa. Pia muongozaji wake Danny Boyle alijitoa kwenye nafasi yake. 
Hivyo kuanza mazoezi kwa mkali huyu mwenye umri wa miaka 50 ni dalili nzuri kwa mashabiki wa filamu hizo ambapo kwa sasa inatayarishwa (Bond 25) itayotoka mwaka 2020. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *