![]() |
Jacob Steven ‘JB’ |
Msanii huyo alisema kwa maisha ya sasa ni lazima kujichanganya katika shughuli tofauti zitakazoleta maendeleo katika maisha ili soko likiyumba mambo yasiharibike.
“Sitegemei filamu pekee kwani hali ya maisha imebadilika, nina biashara zangu za hapa na pale pia nawashauri wasanii wenzangu tusitegemee filamu pekee, tufanye hata biashara ndogo ndogo basi,” alisema JB.
Msanii huyo ameonekana kuwa na hofu ya tasnia ya filamu kuja kufa kutokana na kukosa ubunifu kama ilivyo zamani, hivyo amewataka wasanii wasijisahau.