Mwanaharakati Mzalendo

KAKA AMUUA MDOGO WAKE KWA MADAI YA KUPENDWA SANA NA BABA YAO

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Tarime
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Tarime Rorya Henny Mwaibambe
Mtoto mwenye umri wa miaka 7 Hassan Chacha ambaye ni mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Kitagutiti Kijiji cha Getenga Kata ya Mbogi Wilayani Tarime ameuawa kwa kushambuliwa na kaka yake Mniko Chacha (20) kwa kumning’iniza juu na kumtupa chini.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Tarime Rorya Henny Mwaibambe amesema chanzo cha tukio hilo ni baada ya kaka wa marehemu kudai kuwa mdogo wake anapendwa na baba yao.
“Inasikitisha sana” kaka wa marehemu alimwambia marehemu kuwa “kwanini wewe unapendwa sana,” marehemu huyo ni mapacha Kurwa na Dotto, aliyefariki ni Dotto, “ukiangalia umri wa watoto ni mdogo ni lazima wapendwe tu kaka yao ni mtu mzima hakupaswa kufanya huo ukatili”, alisema Mwaibambe. 
“Alimshambulia na kumning’iniza juu na kumtupa chini mara mbili akidai kwanini anapendelewa na baba yao kwa kuitwa mara kwa mara jikoni, marehemu alipata maumivu ambapo alikimbizwa katika kituo cha Afya cha Dk. Steven na alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu” aliongeza. 
Alieleza kuwa mtuhumiwa alitoroka baada ya kutenda tukio hilo na juhudi za kumtafuta na kumkamata zinaendelea. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *