Mwanaharakati Mzalendo

RAIS MAGUFULI AIKINGIA KIFUA TAIFA STARS

Rais Magufuli amesema kufungwa goli mbili na moja ya timu inayoongoza Afrika ambayo Wachezaji wake wote wanacheza nje si mwanzo mbaya sana ila wasikate tamaa na kujituma zaidi
Aidha, amewasihi Watanzania waendelee kuwaombea kwa sababu kushindwa kwao ni kushindwa kwa Watanzania na ushindi wao ni ushindi wa Tanzania hivyo Watanzania wawasaidie
Katika hatua nyingine amemruhusu Mkuu wa Mkoa wa Dar na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni kwenda Misri kuipa ushawishi Taifa Stars ili iweze kushinda mechi zake
Amesema “Nina kuruhusu(Makonda) nenda, si umesema ukienda tutashinda basi nenda kwa sababu sisi wote tunataka kushinda. Kapande ndege leo, nenda. Ukawaambie Wachezaji wasikate tamaa, kwenye uwanja wa mpira kuna kushinda na kushindwa.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *