Mwanaharakati Mzalendo

Rose Ndauka Alivyowapagawisha Mashabiki wa Soka

STAA wa filamu, Rose Ndauka aligeuka kivutio baada ya mashabiki waliojitokeza kuangalia mchezo wa fainali ya Swaiba Cup, kukacha mtanange huo na kujikuta wakimshangaa.

Rose Ndauka

Mrembo huyo ambaye amewahi kutamba katika filamu mbalimbali za Kibongo, alitimba juzi Uwanja wa Ngunguti, Vikindu Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani kuangalia fainali hiyo ya mpira wa miguu kati ya Ibdhu FC dhidi ya Toyo FC.

Katika fainali hiyo Toyo FC walitwaa taji hilo kwa mikwaju ya penalti 5-3 dhidi ya Ibdhu, lakini stori haikuwa ubingwa huo ni Rose Ndauka.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Rose Ndauka alisema amefarijika kuona vijana wanajituma katika michezo na kuwataka kutimiza malengo yao ya kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL).

Pia, aliwataka wanawake kufuata nyayo za mratibu, Asha Mbata kwa kuandaa michuano ya soka na kuanzisha vituo vya michezo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *