![]() |
Shamsa Ford na Mumewe siku ya Harusi yao |
Shamsa, alisema, kama mwanamke alifurahia kuona anaingia kwenye maisha ya ndoa lakini ilifika wakati akakata tamaa kutokana na mambo mengi aliyoyapitia kwenye maisha hayo hadi kuamua kufanya maamuzi magumu.
Kila mmoja anahitaji mahusiano yenye faida ndani yake na yenye kuheshimika, kwangu siwezi kurudi nyuma na zipo sababu nyingi, ilifika kipindi nikakata tamaa lakini nikasamehe, umefika wakati moyo wangu umekufa ganzi na siwezi kurudi nyuma tenaî alisisitiza Shamsa.
Shamsa ameongeza kuwa kwa sasa ataendelea kufanya mambo yake ikiwemo kusimamia biashara zake pamoja na sanaa yake kama awali kwa kuwa kabla ya hapo alikua ni mwanamke wa kujituma kwa kila jambo.