Wakaguzi nchini marekani wamegundua tatizo jipya katika ndege ya kampuni ya Boeing chapa 737 max ambalo huenda likachelewesha kurudi kuhudumu kwa ndege hiyo.
![]() |
Ndege aina ya BOEING 737 MAX |
Utawala wa safari za anga nchini Marekani-Federal Aviation Administration (FAA) umesema umegundua “inayowezekana kuwa hatari” wakati wa majaribio, lakini haukfichua matokeo.
Ndege hiyo inayouzwa sana katika kampuni ya Boeing ilisitishwa mnamo Machi baada ya ajali mbili za ndege.
Kampuni hiyo inamarisha mfumo wa kutuwa kwa ndege hiyo, ambao unachunguzwa na maafisa wa uchunguzi wa ajali ya ndege.
Katika ujumbe kwenye twitter, FAA limesema: “Katika suala la hivi karibuni, moango wa FAA umeundwa kutambua na kubaini hatari zinazowezekana kuwepo. FAA rhivi karibuni liligundua hatari inayowezekana kuwepo ambayo ni lazima Boeing iitatue.
Mwezi uliopita, FAA liliashiria kuridhia mabadiliko ya Boeing kwa ndege hiyo ya 737 Max ambayo yanaweza kuidhinishwa mwishoni mwa Juni.
Hilo lingeruhusu ndege hizo kufanyiwa majaribio mapema mwezi Julai.
Awali kulikuwa na matumaini kuwa ndege ya 737 Max itarudi angani wakati wamsimu wa joto, lakini mpangilio huo ulisukumwa mwishoni mwa mwaka huu hata kablaya taarifa hii leo.
Reuters, shirika la habari ambalo lilitangulia kuripoti kuhusu tatizo hilo kwanza limesema kuwa wakati wa kufanyiwa majaribio kwa usukani wa rubani ambao mfumo wa kutua uliidhinishwa, ilichukua muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa kupata udhibiti wa ndege hiyo.
Vyanzo vingine vinasema tatizo linahusiana na nguvu ya kompyuta ya ndege hiyo na huenda haukuwa na uwezo wa kupokea maagizo kwa kasi inayohitajika.
Boeing imesema “Tunashirikiana kwa karibu na FAA kuirudisha kuhudumu ndege ya Max ” na kwamba inaamini suluhu kwa mfumo huo utalitatua tatizo lililopo.
Iwapo wakaguzi hawatoridhishwa na suluhu hiyo kw amfumo itabidi ubadilishwe na huenda ikavuta muda wa kurudi kuhudumu kwa ndege hiyo zaidi ya ilivyodhaniwa awali.
Ajali ya ndege ya Ethiopia ET302 mnamo Machi ni ajali ya pili iliyosababisha vifo vya watu iliohusisha ndege yenye chapa ya 737 Max katika muda wa miezi mitano.
Ndege inayokaribia kufanana na hiyo, inayomilikiwa na kampuni ya Indonesia Lion Air, ilianguka baharini kutoka Jakarta mnamo Oktoba 2018.
Ripoti za awali katika ajali zote zimeashiria ajali ilisababishwa na matatizo katika mfumo wa ndege kutua uliochelewa kufanya kazi kwa muda muafaka kutokana na hitilafu katika sensa yake.