Akizungumzia jina hilo Aika amesema mtoto wao huyo wa pili na mpenzi wake Nahreel amepewa jina hilo kutokana na maneno mawili ya Jamila na Aika yaliyozaa Jamaika.
Aika amesema Jamila ni jina la mama yake mzazi, kwamba waliamua kuyaunganisha na kumuita mtoto wao.
“Imekuwa faraja kwa mtoto wetu wa kwanza maana sasa amepata mdogo wake na wanaweza kucheza pamoja,” amesema Aika.