DKT BASHIRU: WAZIRI WA VIWANDA ATATUMBULIWA AKISHINDWA KUFUFUA VIWANDA – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home CCM

DKT BASHIRU: WAZIRI WA VIWANDA ATATUMBULIWA AKISHINDWA KUFUFUA VIWANDA

I am Magnifico by I am Magnifico
Jul 10, 2019
in CCM, DKT BASHIRU, HABARI TANZANIA
0 0
0
DKT BASHIRU: WAZIRI WA VIWANDA ATATUMBULIWA AKISHINDWA KUFUFUA VIWANDA
0
SHARES
49
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Dk Bashiru Ally amesema Waziri wa Viwanda, Innocent Bashungwa atatumbuliwa ikiwa atashindwa kutimiza azma ya Serikali ya kufufua viwanda.
ADVERTISEMENT
Dk Bashiru ametoa kauli hiyo jana Jumanne Julai 9, 2019 baada ya kutembelea kiwanda cha kukoboa kahawa cha TCCCO kilichopo manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.
Amesema ajenda ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kufufua viwanda na kwamba jambo linalopaswa kufanya ni kujiandaa katika masuala ya ushirika, ubunifu na ujuzi ili nchi iweze kujisimamia.
“Nimesoma katika kitabu cha wageni waziri wa Viwanda alikuwa hapa Mei 28 (aliyekuwa Waziri wa Viwanda, Joseph Kakunda) na ameshatumbuliwa, na huyu aliyepo ajiandae kutumbuliwa maana kama tunasema tunahitaji uchumi wa viwanda halafu havifufuki.”
“Barabara zinajengwa unaziona, SGR (Reli ya kisasa) unaiona, kwa nini hatuoni viwanda vinafufuliwa?” amehoji Dk Bashiru.
Amesema kuendesha kiwanda kama TCCCO ni lazima kuwepo na kiwanda cha magunia, “Bado kuna kazi kubwa katika vita ya uchumi, kiwanda hiki ambacho kilitarajiwa kuwa na wafanyakazi zaidi ya 4000 leo kinao 44, mitambo inaitwa mipya lakini haifanyi kazi na imenunuliwa kwa kuuza mali za kampuni, hizi ni hujuma.”
Amebainisha kuwa viwanda vyote vilivyoanzishwa wakati wa Serikali ya Awamu ya Kwanza vina hali mbaya.
Awali akisoma taarifa ya TCCCO, makamu mwenyekiti wa bodi ya kiwanda hicho, Kandata Kimaro amesema kinadaiwa Sh1.2 bilioni na kwamba kahawa inayopokewa kiwandani imeshuka kutoka tani 31,000 mwaka 1988/1989 hadi tani 912 msimu wa mwaka 2018/2019.
Tags: SIASAUCHUMIVIWANDA
ADVERTISEMENT
I am Magnifico

I am Magnifico

Related Posts

Mvua zaleta Majanga Mtwara
HABARI TANZANIA

Mvua zaleta Majanga Mtwara

by Ombeni Osward
Jan 14, 2021
0

Mvua zinazoendele Mtwara zimesababisha watu kukosa makazi...

Read more
ACT Wazalendo yajipanga kutetea Wanufaika wa mikopo ya Elimu ya juu

ACT Wazalendo yajipanga kutetea Wanufaika wa mikopo ya Elimu ya juu

Jan 14, 2021
Waziri ampa siku 7 IGP kushughulikia bajeti ya Mbwa

Waziri ampa siku 7 IGP kushughulikia bajeti ya Mbwa

Jan 11, 2021
Wahitimu Chuo Cha Maji Wanaajirika – Aweso

Wahitimu Chuo Cha Maji Wanaajirika – Aweso

Jan 9, 2021
Dk Ali Mohamed Shein Asimikwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe

Dk Ali Mohamed Shein Asimikwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe

Jan 5, 2021
General wa Jeshi aliemfurumusha Idd Amin Dada Atimiza miaka 101

General wa Jeshi aliemfurumusha Idd Amin Dada Atimiza miaka 101

Jan 4, 2021
Next Post
NEPAL: AFISA WA ZAMANI WA ‘UN’ AFUNGWA JELA KWA KUDHALILISHA WATOTO

NEPAL: AFISA WA ZAMANI WA 'UN' AFUNGWA JELA KWA KUDHALILISHA WATOTO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

July 2019
M T W T F S S
« Jun   Aug »
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031  
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In