Mwanaharakati Mzalendo

INSTAGRAM WAJA NA UPDATE YA KUDHIBITI COMMENTS ZA MATUSI NA KEJELI

Mtandao wa Instagram umefanikisha kuleta Update yake mpya ambayo itasaidia kuondoa Comments za matusi na kejeli ndani ya mtandao huo. Update hii inafanya kazi pale pindi utakapokuwa umekomenti au kutuma ujumbe wa dhihaka, matusi au kejeli kwa mtu fulani, kwa hiyo Instagram kupitia teknolojia yake itakuwa na uwezo wa kutambua neno hilo na kukuzuia kutolituma. 
Ukiachana na hiyo, mlengwa ambae atakuwa amekumbana na komenti hiyo ya matusi atakuwa na uwezo wa kuruhusu mtu huyo komenti zake zionekane au zisionekane, lakini pia atakuwa na uwezo wa kumzuia mtu kutomwona kama Ujumbe wa DM utakuwa umesomwa au haujasomwa na mtu huyo. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *