Mwanaharakati Mzalendo

KENYA: WAZIRI WA FEDHA NA WENZAKE WAFIKISHWA MAHAKAMANI

Waziri wa Fedha wa Kenya, Henry Rotich, Katibu wa wizara hiyo Kamau Thugge na wenzao leo wamepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Milimani kujibu mashitaka yanayowakabili.
Washitakiwa hao wanakabiliwa mashitaka ya ufisadi kwenye ujenzi wa mabwawa Arror na Kimwarer.
Hakimu Douglas Ogoti amesoma mashitaka yanayowakabili na wote wamekana mashtaka.
Miongoni mwa mashitaka yanayowakabili ni matumizi mabaya ya ofisi, kuanzisha mradi bila kuwa na mpango mahususi wa kuutekeleza, kukiuka taratibu za manunuzi na kula njama ili kujipatia fedha kinyume cha taratibu
Rotich anadaiwa kukiuka taratibu za manunuzi na kutoa mkataba wenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani milioni 450 kwa kampuni ya CMC de Ravenna ya Italia ijenge mabwawa hayo.
Mwezi Machi mwaka huu, Rotich alikanusha tuhuma hizo za ufisadi. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *