Mwanaharakati Mzalendo

KUTOKA TWITTER: ELIMU YA KODI (TAXATION) NA MABADILIKO YAKE SEHEMU YA 1

Yafuatayo ni Mabadiliko baadhi katika KODI YA MAPATO (Income Tax):


A: Individual & Corporate Income Tax (Mtu au Kampuni) 

1. Kwa biashara zenye mauzo ghafi “turnover” yasiyozidi million 100 kwa mwaka hawatalazimika tena kuwasilisha hesabu zilizokaguliwa na kuidhinishwa na Wahasibu ili kukadiriwa na kuhakikiwa kiasi cha kodi wanachotakiwa kulipa TRA. 
Zamani kabla ya sheria hii ilikuwa kwamba mfanyabiashara ambae mauzo ghafi katika biashara yalifikia millioni 20 au zaidi, walitakiwa kupeleka TRA hesabu zilizohakikiwa na Wakaguzi/Wahasibu (Audited Financial Statements). 
Kiufupi ni hivi, kwa sasa mfanyabiashara ambae unajua mauzo ghafi “turnover” yanaanzia 0 hadi million 100 kwa mwaka hulazimiki kuwa na mkaguzi wa hesabu zako kwa ajili ya kuwasilisha TRA.
2. SUALA LA KUTAMBULIWA KWA VITAMBULISHO VYA WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO (Machinga). Suala la Vitambulisho vya Machinga linaonekana kutambuliwa/kuzingatiwa na sheria mpya ya Kodi ya Mapato ya 2019/20. Japo haijatajwa moja kwa moja lakini utaona kundi la wafanyabiashara wadogo. 
Ambao mauzo ghafi yao “turnover” hayazidi million 4 kwa mwaka basi watalipa kodi sifuri “0” kule TRA (NIL AMOUNT) Tazama picha kolamu “column” ya kwanza. Hapo chini utaona wenye “turnover” isiyozidi million 4 wanalipa Nil Amount “0”.
Hivyo kwa tafsiri nyepesi ni kwamba kama mauzo ghafi “turnover” kwa mwaka hayazidi million 4 basi kachukue kitambulisho cha WAFANYABIASHARA wadogo wadogo (Machinga) na hapo TRA hawatadai Kodi nyingine.
3. Ahueni kwa Biashara Mpya baada ya kukata TIN. Pia serikali ilipitisha sheria ili kutoa ahueni kwa biashara mpya. Hii ahueni “relief” ya Miezi 6 kwa Wawekezaji na Wafanyabiashara kusubiri kwa kutolipishwa Kodi kwa biashara mpya baada ya kupewa TIN. 
Hii ni tofauti kidogo na zamani ambapo Biashara mpya zilitozwa Kodi wakati wa kupewa TIN bila kujali kwamba biashara haijaanza rasmi na wala haina hata leseni. Sasa utapata TIN na TRA watasubiri miezi 6 ndio waje kukukadiria na kukutoza Kodi. 
4. Mabadiliko baadhi kwa upande wa VAT. 
Sheria ya VAT ya mwaka 2014 pia ilifanyiwa mabadiliko katika vipengele kadhaa:
ENEO LA KILIMO NA MAZAO YAKE: 
Kuondolewa kwa VAT (18%) kwenye uingizwaji nchini wa “Cold room cabinets” au mafriji yanayotumika ktk uhifadhi wa mazao yaharibikayo
Kuondolewa kwa VAT (18%) kwenye uingizwaji wa vifaa vya kukaushia mazao/nafaka. 
Kuondolewa kwa zuio la kurejeshwa kwa gharama za VAT zitokanazo na kuuza mazao ghafi ya kilimo nje ya nchi. 
Ufafanuzi: Kama biashara yako kulima na kuuza nje mazao, gharama za VAT zitokanazo na kilimo hicho hadi wakati wa kuuza nje ya nchi mazao yake zinaweza kurudishwa kwa marejesho ya VAT (Input Tax Credit) hata kama mazao unayouza nje ni ghafi (unprocessed/raw agricultural products)
… Itaendelea siku nyingine kwani bado mengi sana ikiwemo Customs, nk.
CHANZO:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *