Mchezaji wa zamani na mfungaji bora wa muda wa wote wa klabu ya Chelsea – Frank Lampard leo July 4, 2019 ametangazwa rasmi kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo ya jiji la London. Lampard anajiunga na Chelsea kwa mkataba wa miaka 3 akitokea Derby County ya ligi daraja la kwanza.
Anarithi nafasi iliyoachwa wazi na Maurizio Sarri, ambaye ameondoka mwezi uliopita kwenda kujiunga na miamba ya Italia klabu ya Juventus.
Lampard ameiwakilisha Chelsea katika mechi 648 Chelsea, na kunyakua mataji 11 na timu hiyo.