Mwanaharakati Mzalendo

MARVEL yatambulisha Phase 4 ya filamu zao 11 zitakazotoka hivi karibuni

Kama ulifikiri Marvel Studios wameishia kwenye ‘Avengers:Endgame’, basi umepuyanga sana. jana mjini San Diego Marekani, kampuni hiyo ya filamu imetangaza ujio wa filamu zao 11 ndani ya miaka miwili. 
Phase 4 ya filamu hizo imetangazwa ndani ya Hall H ambapo pia vipindi vipya vya televisheni vilipata kutambulishwa.
1. Eternals – Ni filamu ambayo imemkutanisha mwanamama Angelina Jolie ambaye ametangazwa rasmi leo kujiunga na Marvel na atahusika kwenye filamu hii ambayo itaongozwa na Chloé Zhao na itaingia kwenye majumba ya sinema November 6, 2020.
2. The Falcon And The Winter Soldier – Hii itatoka mwishoni mwa mwaka 2020.
3. Shang-Chi And The Legend Of The Ten Rings – Chini ya muigizaji mkuu Simu Liu. Hii itaingia kwenye majumba ya sinema February 12, 2021.
4. Wanda Vision – Hii itatoka kati ya March na April, 2021.
5. Loki – Hii itatoka sambamba na Wanda Vision.
6. Doctor Strange In The Multiverse Of Madness – Chini ya mwigizaji Benedict Cumberbatch kama Stephen Strange akiwa na muongozaji Scott Derrickson. Hii itatoka Mei 7, 2021.
7. WHAT IF…? Filamu hii ya kwanza ya uhuishaji (animated series) ndani ya Marvel Comics Universe itatoka 2021.
8. Hawkeye – Itatoka 2021.
9. Thor: Love and Thunder – Hii itatoka November 5, 2021.
10. Black Widow – Itatoka Mei 1, 2020.
11. Blade – Hii ina Good News kwani imepata mwigizaji mpya, Mahershala Ali ndio atakuwa Blade kwenye filamu hii ambayo haijawekwa tarehe ya kuachiwa rasmi. Blade awali ilikuwa inachezwa na Wesley Snipes. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *