Mwanaharakati Mzalendo

MWANZA: POLISI WALIOSINDIKIZA DHAHABU WAFUTIWA MASHTAKA

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DDP) Biswalo Mganga, amewafutia kesi askari Polisi nane waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba moja ya mwaka 2019 iliokuwa ikiunguruma katika Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mwanza. 

Biswalo alisema pamoja na kuwafutia askari hao kesi hiyo pia amefuta kesi nyingine 322 katika magereza saba ya mikoa ya kanda ya ziwa kwa maslahi mapana ya umma.

DPP ametangaza uamuzi huo jijini Mwanza, mara baada ya kukamilisha ziara yao ya kutembelea mahakama za mikoa hiyo, ambapo waliambatana na Waziri wa Sheria na Katiba, Balozi Agustino Mahiga na viongozi mbalimbali wa Serikali.

Biswalo alisema kuwa serikali imeamua kufuta kesi hizo 323 ikiwemo ya Askari Polisi hao waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa maslahi mapana ya umma na kwamba serikali imeona hakuna sababu na umuhimu wa kuendelea na kesi hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *