Mwanaharakati Mzalendo

PAMOJA NA KULALAMIKIWA NA WASWAHILI, ‘THE LION KING’ YAFANYA VIZURI SOKONI

Achana na kelele za Watanzania na watu wa Afrika Mashariki kuhusu kukosekana kwa wasanii wa Ukanda huo kwenye album mpya ya Beyonce mahususi kwa ajili ya filamu ya ‘The Lion King’, kuna habari njema kwa wapenzi wa filamu hiyo.The Lion King imefanikiwa kuingiza jumla ya $185 Million sawa na TZS Bilioni 426 katika wikiendi yake ya kwanza tu kwenye Soko la Amerika ya kaskazini na $531 Million sawa na TZS Trilioni 1 duniani kote.


Hii inaifanya kuweka rekodi ya kuwa filamu yenye mauzo makubwa kwa muda wote katika kipindi cha uzinduzi wa filamu za kutazamwa na usaidizi wa wazazi yaani PG film. Pia ya 9 katika filamu zote. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *