![]() |
Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania na Uhuru Kenyatta wa Kenya |
Ameyasema hayo leo Ijumaa Julai 5, 2019 baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita Tanzania kwaajili ya ziara binafsi ya siku mbili.
“Mimi kama kiongozi wa Kenya nimesema kama kuna kitu ningependa nione mbele ya wakati wangu, ni sisi wana Jumuiya ya Afrika Mashariki tukiwa kitu kimoja” amesema Rais Kenyatta akihutubia wananchi
Amesema Tanzania na Kenya ni marafiki hivyo viongozi wanapaswa kuhakikisha wanaondoa vikwazo katika mwingiliano kwa nchi hizo mbili.
“Hakuna kitu ya furaha kama kuwa una jirani uliyechaguliwa na mwenyezi Mungu na pia huyo jirani ni rafiki na ndio tuko hapa kuimarisha huo urafiki” amesema
“Ndio tuko hapa kusisitiza ya kwamba mataifa yetu mawili, sisi kama watoto wa Afrika Mashariki twasema yastahili hasa sisi viongozi kufanya yote ambayo tunaweza, kuhakikisha ya kwamba tumeondoa vikwazo vyote ambayo vyazuia vinavyozuia watu wetu kutembeleana, kufanya biashara pamoja, kuoana” amesema
Amesema njia ya kuimarisha ujirani ni kuondoa mambo yanayoweza kuharibu urafiki.
“Wajua njia ya kumaliza ukabila na mipaka ni watu waoane, hiyo ndo njia ya kumaliza ukabila na mambo mengine ambayo yanatugawanya,” amesema
Rais Kenyatta ambaye amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Chato saa 8:45 mchana amepokelewa na mwenyeji wake, Rais wa Tanzania John Magufuli.
Akiwa Chato, Rais Kenyatta atafanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Magufuli
Rais Kenyatta amekuja nchini baada ya kualikwa na mwenyeji wake Rais Magufuli na kesho Jumamosi atamaliza ziara yake na kurejea nchini kwake.