Mwanaharakati Mzalendo

SAKATA LA INTER NA ICARDI; ICARDI AONDOKA KAMBINI SWITZERLAND

Mshambuliaji Mauro Icardi hatosafiri na klabu ya Inter kwenda Asia baada ya kuondoka kambini kwa makubaliano yake na timu hiyo. 
Icardi
Juzi Jumamosi klabu ya Inter kupitia ukurasa wao katika mtandao wa Twitter walitoa taarifa ya mshambuliaji huyo kurejea Milan akitokea katika kambi ya timu hiyo Switzerland na hivyo hatakuwa na kikosi chao kinachoenda Asia kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya. 
Mshambuliaji huyo wa Argentina hayupo katika mipango ya kocha mpya wa Inter Milan Antoine Conte, ikiripotiwa kuwa anatarajiwa kuuzwa. 
Icardi (26) ambaye alivuliwa unahodha wa Inter Milan msimu uliopita, anahusishwa kutakwa na Juventus, huku klabu za Man United na Napoli pia zikimmendea. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *