Msanii wa vichekesho nchini Tanzania, Brian Mrikaria ‘Mr Beneficial’ amesema nguo anazozivaa wakati wa kuigiza sio kubwa.
![]() |
Brian Mrikaria ‘Mr Beneficial’ |
Akizungumza na gazeti la Mwananchi, amesema kwake viatu na nguo vyote anavyovaa ni saizi yake.
Huku akieleza kuwa kwa watu wanaomuona kwamba kavaa viatu ‘oversize’ wajue kwamba vinambana.
Wakati kwa wale wanaoona kavaa nguo kubwa kuzidi mwili wake, wao macho yao ndio makubwa na sio nguo zake.
Mr Beneficial ni kati ya wachekeshaji walioteka mitandao ya kijamii kwa sasa kutokana na staili yake ya uigizaji huku kubwa ikiwa kuongea lafudhi ya watu wa pande za Arusha.
Kampuni Timamu, anayofanya nayo kazi kwa sasa, ndio iliyomrudisha kwenye soko la sanaa ya uigizaji, marehemu King Majuto na kumpa umaarufu marehemu Sharomilionea.