Tanzania yapokea Dhahabu na Fedha Zilizokamatwa Kenya – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home BONGO MOVIE

Tanzania yapokea Dhahabu na Fedha Zilizokamatwa Kenya

I am Magnifico by I am Magnifico
Jul 24, 2019
in BONGO MOVIE, BURUDANI, IRENE UWOYA
0 0
0
Tanzania yapokea Dhahabu na Fedha Zilizokamatwa Kenya
0
SHARES
76
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
Serikali ya Tanzania imepokea kilo 35.34 za madini ya dhahabu zenye thamani ya dola milioni moja za Marekani na fedha kiasi cha shilingi milioni 170 za Tanzania, dola za Marekani 76,500 na shilingi za kenye 171,600, fedha zilizokamatwa nchini Kenya.

Waziri wa mambo ya nje wa Kenya, Monica Juma akizungumza 

Mali hiyo ilikamatwa tangu mwaka 2004 baada ya kuibwa kwenye benki ya NBC tawi la Moshi.

Ujumbe wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ukiongozwa na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo, Monica Juma na Mkurugenzi wa mashtaka Nurdini Haji, umekabidhi madini na fedha hizo Ikulu ya Tanzania na kutoa ripoti kuhusu namna madini hayo yalivyokamatwa mwaka jana nchini Kenya.

Mkurugenzi wa mashtaka wa Tanzania, Biswalo Mganga, aliongoza timu ya watu 11 kuhakikisha dhahabu iliyokamatwa inarejea ili kuweza kutumika kama kidhibiti kwenye kesi inayoendelea kuhusu makosa ya uhujumu uchumi huko Mwanza.

”Mnamo tarehe 15.2.2018 dhahabu ya kilo 35.34 wakati msafiri mmoja ajulikanaye kwa jina la Baraka Chaulo aliyesafiri na ndege ya shirika la Presicion akitokea jijini Mwanza, kisha kutua Kilimanjaro na baadae kuelekea Kenya alipokamatwa kwenye uwanja wa Jommo Kenyatta..taarifa zilipopatikana, mkurugenzi wa upelelezi wa Tanzania na mwenzake wa Kenya walishirikiana kufanyia upelelezi tukio hilo”.

Mganga amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Profesa Adelardus Kilangi aliandika maombi kwenda Kenya kuomba dhahabu hiyo irejeshwe.

Amesema pia taratibu za kumrejesha nchini kutoka Kenya mtu aliyeshiriki uvamizi katika benki ya NBC tawi la Moshi zilikwama kwa miaka mingi, lakini kwa ushirikiano kati yake na DPP wa Kenya, mshtakiwa huyo ameshejeshwa Tanzania na kesi yake iko Moshi.

Sheria za Usimamizi wa Forodha za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) za mwaka 2004, kifungu 85(3) na Kiambatanisho cha Pili Sehemu B (4) huharamisha usafirishaji wa madini ambayo hayajapitia viwandani katika kanda ya Afrika Mashariki.

Naye Rais Magufuli baada ya kukabidhiwa dhahabu na fedha ameshukuru serikali ya Kenya kutekeleza jambo hilo.

“Namshukuru Rais Kenyatta kwa upendo na uaminifu mkubwa alionao kwa kurejesha dhahabu yenye uzito wa kilo 35 pamoja na fedha, rais Uhuru amefanya kitendo cha kiungwana kwa kuturudishia madini yetu ambayo yalikuwa yametoroshwa.

“Navipongeza vyombo vya ulinzi na usalama vya Kenya kwa kazi kubwa walioifanya.”Tuliamua kuchukua hatua za makusudi za kuweka mikakati ya kulinda rasilimali zetu za madini ili ziweze kuwanufaisha Watanzania”

Kwa mujibu wa rais Magufuli matukio ya utoroshaji wa madini nchini Tanzania yamefika 102 kwa mwaka uliopita pekee.

“Wa kupongezwa kwa hili ni vyombo vya Kenya, najua wakuu wa vyombo hivyo Tanzania mpo hapa, lazima niwatandike kwa sababu vitu vimetoka Mwanza vimekamatiwa Kenya. Je, vilipobebwa Mwanza na Kilimanjaro vyombo vyetu vilikuwa vinafanya nini?

‘Vitu vya fedha na dhahabu vinahitaji moyo wa jiwe, kiukweli Rais Kenyatta ni muaminifu, kwani vingeweza kupigwa, lakini fedha hizi zimerudi Tanzania baada ya miaka 15. Lakini na mimi mnipongeze, inawezekana wengine wangepiga dili juu kwa juu na wala msingejua.

Raisi John Magufuli azungumza na raisi Uhuru Kenyatta kwa simu

Ilikuwa hafla iliyosisimua kwani wakuu hawa wa nchi walizungumza kwa simu, baada ya Uhuru Kenyatta kumpigia Magufuli moja kwa moja wakati wa hafla hiyo.

Awali, Magufuli alimpigia simu Kenyatta lakini hakupokea, wakati akiendelea kuzungumza na viongozi mbalimbali waliokuwa wakishuhudia tukio la makabidhiano.

”Naona Kenyatta ananipigia,kumbe ameshapiga mara nyingi, maneno nayo ni matamu saa nyingine unasahau”. alisema Magufuli akiwavunja mbavu viongozi waliokuwa wakimsikiliza.

Rais Magufuli: Halooo

Rais Kenyatta: Mheshimiwa rais habari ndugu yangu?

Rais Magufuli: Nzuri bwana, mzigo umeshafika, mimi ninakushukuru sana.

Rais Kenyatta: Asante asante asante, tumesema kwamba mali ya wananchi wetu irudi kwa wananchi wetu.

Rais Magufuli: Sawa kabisa, endelea wanakusikiliza hapa.

Rais Kenyatta: Tumesema kwamba sisi kazi yetu ni kuhakikisha tumelinda mali za wananchi wetu na mali hiyo iweze kuwajengea wananchi hospitali, barabara, shule. Walaghai hawana nafasi kwa nchi zetu kabisa.

Rais Magufuli: Safi kabisa.

Rais Magufuli ameahidi kuwapatia zawadi wanausalama waliofanikisha juhudi za kukamtwa kwa wahalifu hao.

ADVERTISEMENT
I am Magnifico

I am Magnifico

Related Posts

Wateja wa Tigo Zanzibar kulipa bili za maji kwa Tigo Pesa
BURUDANI

Wateja wa Tigo Zanzibar kulipa bili za maji kwa Tigo Pesa

by I am Krantz
Jan 14, 2021
0

MAMLAKA ya Maji Visiwani Zanzibar (ZAWA), kwa...

Read more
Maisha Magic Bongo yazidisha uhondo wa Burudani

Maisha Magic Bongo yazidisha uhondo wa Burudani

Jan 6, 2021
WAZIRI BASHUNGWA AUNGANA NA MAMIA YA MASHABIKI  KATIKA TAMASHA LA XXL UNI BASH 2020

WAZIRI BASHUNGWA AUNGANA NA MAMIA YA MASHABIKI KATIKA TAMASHA LA XXL UNI BASH 2020

Dec 20, 2020
Harmonize hataki tumsifie Diamond-Baba levo

Harmonize hataki tumsifie Diamond-Baba levo

Dec 14, 2020
Kamishina  wa Bima aipongeza Benki ya CRDB kuanzisha huduma ambatanishi ya bima kwa wateja

Kamishina wa Bima aipongeza Benki ya CRDB kuanzisha huduma ambatanishi ya bima kwa wateja

Dec 7, 2020
SHUHUDIA KIVUMBI TIMU YA DSTV NA KCB, WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

SHUHUDIA KIVUMBI TIMU YA DSTV NA KCB, WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

Oct 10, 2020
Next Post
MEEK MILL ASHIRIKIANA NA JAY Z KUANZISHA LEBO YAKE

MEEK MILL ASHIRIKIANA NA JAY Z KUANZISHA LEBO YAKE

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

July 2019
M T W T F S S
« Jun   Aug »
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031  
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In