Mwanaharakati Mzalendo

Tetesi za soka Ulaya leo Jumanne: Rojo, Neymar, Lukaku, Milinkovic-Savic, Dybala

Inter Milan bado wanaufanyia kazi mkataba wa mshambuliaji Mbelgiji Romelu Lukaku licha ya kuweza kupata mkataba na Manchester United kwa ajili ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 26. (Sky Sports)
Mlinzi wa Argentina Marcos Rojo, mwenye umri wa 29, ataangalia uwezekano wa kuondoka Manchester United ikiwa anaamini fursa za timu ya kwanza itakuwa ndogo kwa msimu ujao. (ESPN)


Rais wa Lazio Claudi Lotito amefichua kuwa yuko wazi kwa wazo la kumuuza kiungo wa kati wa Serbia -Sergej Milinkovic-Savic, mwenye umri wa miaka 24 anayelengwa na Manchester United ikiwa wataombwa kufanya hivyo. (Mail)


Mchezaji mwenza wa Neymar katika kikosi cha Paris St-Germain Marco Verratti anakiri kuwa klabu hiyo lazima imuuze mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27- raia wa Brazil ikiwa hana raha katika Parc des Princes, licha ya kocha Thomas Tuchel wa kutaka mchezaji huyo abaki kikosini. (Express)


Juventus amethibitisha kuwa kumekuwa na ofa kwa ajili ya mshambuliaji wake raia wa Argentina Paulo Dybala, huku kukiwa na nia ya kumnunua mchezaji huyo kutoka kwa Manchester United na Tottenham ya kumnunua . (Mirror)


Real Madrid wamemuambia mshambuliaji wa safu ya kati wa MColombia James Rodriguez, mwenye umri wa miaka 28, kwamba atakuwa katika Bernabeu. (AS – in Spanish)


Crystal Palace wamepanga kuwasilisha dau la pauni milioni 5 la kutaka kumnunua mchezaji wa Newcastle na Jamuhuri ya Ireland anayecheza safu ya kati nyuma Ciaran Clark, mwenye umri wa miaka 29. (sun)


Everton wanaangalia uwezekano wa kumhamisha kiungo wa kati wa Southampton na Gabon Mario Lemina, mwenye umri wa miaka 25, pamoja na mchezaji wa Chelsea na England kutoka kikosi cha vijana wenye umri wa chini ya miaka -21 Fikayo Tomori, mwenye 21 anayecheza katika safu ya ulinzi . (Sky Sports)


Meneja wa Newcastle Steve Bruce haamini kuwa mashabiki wa klabu hiyo watasusia mechi ya kwanzaya msimu dhidi ya Arsenal. (Talksport)


Swansea City wanaangalia uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa Mskochi Oli McBurnie mwenye umri wa miaka 23 kutoka Sheffield United. (Wales Online)


Real Madrid wamepokea ofa kutoka kwa Roma na Monaco kwa ajili ya mshambuliaji wa Dominican Mariano, mwenye umri wa miaka 25. (AS – in Spanish)


Lille wanaangalia uwezekano wa kuwaajiri washambuliaji wawili au watatu kwa Euro milioni 115 (£104m) wanazotarajia kuzipata kutokana na mauzo ya wachezaji Nicolas Pepe na Rafael Leao. (RMC Sport – in French)


Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Ujerumani Jurgen Klinsmann, mwenye umri wa miaka 55 Jumanne anafanya mazungumzo na VfB Stuttgart ili kuwa mkurugenzi wao mkuu wa kwanza kabisa. (Bild – in German)


Mlindalango wa Real Madrid Thibaut Courtois, mwenye umri wa miaka 27, hana uhakika kuhusu mwango wa La Liga baada ya kuumia kiwiko . (Evening Standard)


kiungo wa kati wa Ireland midfielder Sam Foley,mwenye umri wa miaka 32,ambaye ni wakala huru ,anakamilisha taratibu za kuhamia St Mirren. (Record)


Mchezaji wa kiungo cha kati wa Sporting Lisbon Bruno Fernandes, mwenye umri wa miaka 24, hatarajiwi kusafiri kwenda England kufayiwa ukaguzi wa kimatibabu na Manchester United. (Daily Express)


Winga wa Lille Nicolas Pepe, mwenye miaka 24, atakamilisha uhamisho wake wa thamani ya £72m kwenda Arsenal Jumanne au Jumatano -ili mradi mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain hawatojaribu kuteka makubaliano hayo. (La Voix Du Nord)


Mchezaji wa kiungo cha kati wa Juventus Blaise Matuidi, mwenye umri wa miaka 32, ana hamu ya kuelekea Manchester United. (Corriere di Torino kupitia Daily Express)


Everton imewasilisha ombi la £55m pesa taslimu kumsajili mchezaji wa kiungo cha mbele wa Crystal Palace Wilfried Zaha huku kukiwa hakuna mchezaji wanayejitolea kubadilishana na wapinzani wao katika Premier League. (Sky Sports)


Palace inataka £60m awali ili kumuachia mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast na pia ina wasiwasi kuhusu namna Everton inavyotaka kupangia malipo katika makubaliano yoyote yanayowezekana kuidhinishwa. (Daily Mirror)


Mchezaji wa kiungo cha kati wa Everton Idrissa Gueye, mwenye umri wa miaka 29, amepigwa picha akiwasili katika uwanja wa ndege Paris wakati mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal akikaribia kuelekea kujiunga na mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain. (RMC Sport kupitia Liverpool Echo)


Liverpool inapanga kumjumuisha winga mwenye miaka 16 Harvey Elliott katika kikosi cha kwanza msimu huu badala ya kumjumuisha na kikosi cha kinachopokea mafunzo kufuatia uhamisho wake kutoka Fulham. (Liverpool Echo)


Aston Villa imehimizwa katika kumtafuta kwao kwa kipa wa Cardiff City Neil Etheridge, mwenye umri wa miaka 29, baada ya bosi wa Bluebirds Neil Warnock kusema klabu hiyo ipoa tayari kusikiliza maombi. (Wales Online)


Watford ingali katika mazungumzo na klabu ya Ufaransa Rennes kuhusu kiungo cha mbele wa Senegal, Ismaila Sarr, mwenye miaka 21, licha ya kwamba makubaliano ya gharama yanadhaniwa kukaribia kukamilika.(Watford Observer)


Winga wa Liverpool Ryan Kent hatoondoka Anfield tena kwa mkopo, na kuipa pigo matumaini ya timu bingwa ya Uskotchi Rangers ya kumsajili mchezaji huyo wa miaka 22 katika mgeuzi mengine ya muda mfupi. Hilo huenda likatoa fursa kwa Aston Villa au Leeds United kumpata Kent katika uhamisho wa £10m. (Daily Record)


Mabingwa Blackburn Rovers bado wana imani ya kumsajili beki wa kati wa Manchester City Tosin Adarabioyo, mwenye miaka 21, kwa mkopo wa msimu mzimu huku mchezaji wa Fortuna Dusseldorf Robin Bormuth, mwenye umri wa miaka 23, na wa Norwich Grant Hanley, wa miaka 27, huenda pia wakawasili. (Lancashire Telegraph)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *