Mwanaharakati Mzalendo

Tetesi za soka Ulaya Leo Ijumaa: Bale, Griezmann, Lukaku, Koscielny, Fernandes, Diaz

Barcelona inakaribia kumsaini mshambuliaji wa Ufaransa na Atletico Madrid Antoine Griezmann kutoka Atletico Madrid kwa dau la £107m . (Mirror)

Duru kutoka Barcelona zimekana ripoti kwamba tayari klabu hiyo imetoa dau hilo (Sport)

Mshambuliaji Gareth Bale, 29, alishiriki mazoezi na wenzake wa Real Madrid nchini Canada huku akiendelea kujilazimisha katika mipango ya mkufunzi Zinedine Zidane. (Mail)

Newcastle inajiandaa kumteua mkufunzi wa Sheffield Wednesday Steve Bruce kuwa kocha wake na wanatumai ataweza kujiunga na timu hiyo katika maandalizi ya msimu ujao ziarani China. (Telegraph)

Newcastle inajadiliana kuhusu fidia ya takriban £5m na klabu ya Sheffield Wednesday ili kumsajili Bruce. (Times)

Manchester United na Manchester City zimepigwa jeki katika harakati za kumsajili Bruno Fernandes huku klabu yake ya Sporting Lisbon ikikaribia kumsajili mchezaji atakayechukua mahala pake.. (Mirror)

Manchester United imeanza majadiliano na Roma kuhusu kumuuza mshambuliaji wake mwenye umri wa miaka 26 Romelu Lukaku. (Goal.com)

Mkurugenzi wa michezo katika klabu ya Inter Milan Piero Ausilio amesafiri kuelekea mjini London ili kukutana Manchester United ili kuona iwapo dau watakaloliwakilisha kumsajili Lukaku litafanikiwa kumnunua (Guardian)

Ajenti wa beki wa Tottenham Toby Alderweireld amefanya mazungumzo na Roma kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 mwenye thamani ya £22.5m. (Calciomercato)

Mchezaji wa Real Madrid na Jamhuri ya Dominican Mariano Diaz, 25, hana hamu ya kujiunga na Arsenal msimu huu. (AS, via Mirror)

Paris St-Germain wanatarajiwa kuimarisha hamu yao ya kutaka kumsajili mchezaji wa Everton Idrissa Gueye kwa dau la £27m kwa kiungo huyo wa Senegalr. (L’Equipe, via Sun)

Arsenal ina hamu ya kumsajili mchezaji wa Real Madrid’s Dani Ceballos kwa mkopo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 pia amekuwa akifanya mazungumzo na klabu ya Tottenham. (Sky Sports)

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp anatarajiwa kuzuia jaribio la Steven Gerrard kumrudisha winga Ryan Kent katika klabu ya Rangers msimu huu. Mchezaji hyo mwenye umri wa miaka 22 alihudumu msimu uliopita kwa mkopo na klabu hiyo ya Uskochi.. (Express)

Ajenti wa winga wa PSV Eindhoven Steven Bergwijn, 21, ameiambia klabu ya Bayern Munich kwamba mteja wao anayekumbwa na uvumi wa kuhamia klabu ya Manchester United yuko tayari kuhamia Ujerumani. (Express)

Manchester United wamefutilia mbali hamu yao inayoripotiwa ya kumsaini mchezaji wa Southampton na Gabon Mario Lemina, 25, ambaye amehusishwa na Arsenal. (Manchester Evening News)

Mshambuliaji wa Bournemouth na Uingereza Callum Wilson, 27 – anayelengwa na West Ham – anatarajia kutia saini mkataba mpya wa miaka minne na The Cherries. (Talksport)
Bournemouth inajiandaa kumruhusu mchezaji mwenye umri wa miaka 25 winga wa Uskochi Ryan Fraser, ambaye amehusishwa na uhamisho wa Arsenal, kuondoka kwa dau la bila malipo mwisho wa msimu ujao badala ya kumuuza msimu huu. (Express)

Mchezaji wa zamani wa Uingereza Peter Crouch, 38, hajaamua iwapo atastaafu baada ya kandarasi yake na Burnley kuisha msimu huu . (Talksport)

Wachezaji wanaolengwa na Newcastle Joelinton, mchezaji wa Hoffenheim ,22 raia wa Brazil pia ananyatiwa na Wolves. (Newcastle Chronicle)

Winga wa Crystal Palace 26 Wilfried Zaha, ambaye amehusishwa na uhamisho wa kuelekea Arsenal hakushirikishwa katika picha za jezi mpya ya ugenini ya klabu hiyo. (Express)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *