Kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen,27, ni moja ya majina yaliyowekwa wazi na Atletico wakiwa wanatazamia kumsajili mchezaji huyo. (Evening Standard)
Mlinzi wa kushoto wa timu ya taifa ya England Danny Rose, 29, hatasafiri na Spurs kwenda Singapore, huku ikielezwa kuwa yuko sokoni. (Telegraph)
Manchester United imetoa ofa ya donge nono kumnyakua kiungo Bruno Fernandes, 24, wa Sporting Lisbon. (Mirror)
Barcelona wana mpango wa kumsajili beki wa kushoto Junior Firpo, 22, wa Real Betis kuziba nafasi ya Jordi Alba. (Marca)
William Saliba anataka kuhamia Arsenal lakini timu yake , St Etienne imevutiwa na ofa ya tottenham kwa mchezaji huyo wa miaka 28. (the sun)
Cardiff City imepiga hatua muhimu ya kutaka kufanya mazungumzo na klabu ya Bordeaux ya ufaransa kuhusu mchezaji Younousse Sankhare,29, baada ya kuachwa kwa kiungo huyo na timu yake katika mechi za maandalizi ya msimu mpya nchini Marekani. (Wales Online)
Mchezaji wa nafasi ya ulinzi ya Atalanta Gianluca Mancini anajiandaa kuhamia Roma kwa kitita cha pauni milioni 26. (Gazzetta dello Sport )
Parma imemsajili tena mshambuliaji Roberto Inglese, 27, kutoka Napoli kwa mkopo- ingawa klabu hiyo inawajibika kumnunua. (Corriere dello Sport – in Italian)
Liverpool imemjumuisha Andy Linergan, 35, kwenye mechi za maandalizi, Amerika Kaskazini kuziba nafasi ya mlinda mlango. . (Daily Mail)