Barcelona inataka kumsajili tena Neymar kutoka PSG, (Sport, via Express)
Kiungo wa Fulham Jean Michael Seri anajiandaa kujiunga na Galatasaray ya Uturuki kwa mkopo. (Mail)
Kocha wa Chelsea Frank Lampard ataamua kuhusu mchezaji Willian kama atapata mkataba mpya katika klabu hiyo. winga huyo, 30, amebakisha mwaka mmoja na Barcelona inamtaka mchezaji huyo kwa kitita cha pauni milioni 30. (Express)
Kocha mkuu wa Newcastle United Steve Bruce anaweza kutumia zaidi ya pauni milioni 90 katika dirisha la usajili. (Sky Sports)
Bruce ‘alikuwa chaguo la 11’ kwa ajili ya kazi hiyo ndani ya Newcastle. (Daily Mail)
Mshambuliaji wa zamani wa Newcastle Alan Shearer amesema alimwambia Bruce kutochukua kazi ya ukocha kwenye klabu . (Sun)
Hoffenheim wamethibitisha kuwa mshambuliaji Joelinton, 22, yuko kwenye ”mazungumzo ya kina” na klabu hiyo na Newcastle United wana matumaini ya kuvunja rekodi kumnasa mchezaji huyo mwenye asili ya Brazil. (Chronicle Live)
Kocha wa Leicester Brendan Rodgers ameitahadharisha Mnchester kuwa kuna muda wa ukomo ikiwa wanataka kumsajili Harry Maguire, 26, (Star)
Kocha wa Leicester Brendan Rodgers amesifu utaalamu wa Harry Maguire, 26, na kukubali kuwa alikuwa ”ametulia” kuhusu nia ya Manchester United kumnasa mlinzi huyo wa kati .(Independent)