Mwanaharakati Mzalendo

UKUAJI WA UCHUMI TZ 2018: BENKI YA DUNIA YATOFAUTIANA NA SERIKALI

Uchumi wa taifa la Tanzania ulipanuka kwa asilimia 5.2 mwaka 2018 kulingana na benki ya dunia iliosema katika katika ripoti yake kuu mwaka huu ambapo imetofautiana na takwimu zilizotolewa na serikali hiyo za kuimarika kwa uchumi huo.
Kulingana na chombo cha habari cha Reuters, waziri wa fedha nchini Tanzania alikuwa ameliambia bunge mwezi uliopita kwamba ukuwaji huo ulikuwa wa asilimia 7 mwaka uliopita. 
Katika ripoti hiyo, kulingana na Reuters, benki kuu ya dunia ambayo hufanya hesabu zake kwa kutumia data ilizonazo pia ilikadriria kwamba uchumi huo utakua kwa asilimia 5.4 ikiwa ni chini ya asilimia 7.1 inayokadiriwa na serikali.
Ukuaji wa mwaka uliopita uliathiriwa na kushuka kwa viwango vya uwezekazji, mauzo katika mataifa ya kigeni na ukopeshaji katika sekta ya kibinfasi, ripoti hiyo imesema.
Kulinga na Reuters, data inayohusiana na matumizi, uwekezaji na biashara inonyesha kwamba ukuaji huo ulipungua mwaka 2018, imesema ripoti hiyo.
Rais John Pombe Magufuli alianzisha mpango wa kuimarisha sekta ya viwanda baada ya kuchukua hatamu mwaka 2015, akiwekeza mabilioni ya dola katika miundo msingi, ikiwemo barabara ya reli, kufufua uchukuzi wa kitaifa wa angani pamoja na kiwanda cha umeme.
Lakini hatua ya serikali kuingilia sekta ya uchimbaji wa madini pamoja na ile ya kilimo imesababisha kupungua kwa uwekezaji katika sekta hizo katika taifa hilo linalotajwa kuwa la tatu kwa ukubwa kiuchumi Afrika mashariki, ilisema ripoti hiyo iliochapishwa na Ruters.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *