Mwanaharakati Mzalendo

WAZIRI LUGOLA ARUHUSU MABASI YA ABIRIA KUSAFIRI MASAA 24

Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amepiga marufuku Makamanda wa Polisi wa mikoa nchini kuzuia mabasi yanayofanya safari katika ya Jiji la Dar es Salaam na Mikoa ya Kanda ya Ziwa kusafiri usiku kwa kisingizio cha kuhofia kuvamiwa na majambazi. 
Ametoa kauli hiyo jana Jumapili Julai 7, 2019 katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na Wananchi wa vijiji vya Namibu na Mwibara wilayani Bunda mkoani Mara. 
Taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo imemnukuu mbunge huyo wa Mwibara(CCM) akisisitiza kuwa mabasi yanayotoka mikoa ya Kanda ya ziwa kwenda Dar es Salaam kutozuiwa mkoani Morogoro na yanayotoka Dar es Salaam kwenda katika mikoa hiyo kutozuiwa yanapofika mkoani Shinyanga. 
“Hatuwezi kupangiwa ratiba ya kusafiri na majambazi, Serikali ipo imara pamoja na Polisi. Niliwahi kutoa agizo majambazi wote wasambaratishwe, asakwe hadi jambazi wa mwisho na akamatwe kama kuku.” 
“Taarifa za uhalifu zinaonyesha Polisi imefanya kazi kubwa kupambana na uhalifu na hasa majambazi, niliwahi kusema kipindi hiki si cha huruma na majambazi bali cha kuhakikisha Wananchi wanaishi kwa amani,” amesema Lugola. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *