Ajuza Wa Miaka 98 Kulipwa Milioni 519.30 Kama Fidia Ya Kuporwa Ardhi Yake Arusha – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home Arusha

Ajuza Wa Miaka 98 Kulipwa Milioni 519.30 Kama Fidia Ya Kuporwa Ardhi Yake Arusha

I am Magnifico by I am Magnifico
Aug 29, 2019
in Arusha, HABARI TANZANIA
0 0
0
Ajuza Wa Miaka 98 Kulipwa Milioni 519.30 Kama Fidia Ya Kuporwa Ardhi Yake Arusha
0
SHARES
73
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT
Hatimaye kaya 109 zimetakiwa kumlipa fidia jumla ya Sh519.3 milioni kikongwe Nasi Muruo(98) mkazi wa eneo la Sinoni, katika jiji la Arusha, baada ya kurejeshwa ardhi yake aliyokuwa anaidai kwa miaka 42 .
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ametangaza jana Jumatano Agosti 28,2019 uamuzi huo wakati akizungumza na kaya hizo na bibi Muruo katika viwanja vya shule ya msingi Sinoni.
Lukuvi alikuwa ameandamana na mkuu wa wilaya Arusha, Gabriel Daqaro na maofisa ardhi katika kutatua mgogoro huo.
Amesema kila kaya italipa kiasi cha Sh20,000 kwa mita moja ya mraba katika eneo la bibi huyo, lakini italipia pia fedha za kupimwa ardhi ili kupewa hati ndani ya miezi mitatu
Kikongwe huyu alirejeshewa ardhi yake, Julai 8, 2019 na Waziri Lukuvi, kutokana na maelekezo ya Rais John Magufuli wa Tanzania, alipomtaka kushughulikia mgogoro huo, hasa baada ya kuripotiwa malalamiko ya Kikongwe huyo, kunayanyang’anywa ardhi yake tangu mwaka 1977 na ndugu wa ukoo wao, Edward Lenjeshi 
Akizungumza na Mwananchi, Nasi Muruo ameshukuru Rais Magufuli na Lukuvi kwa uamuzi huo ambao umeugwa mkono na pande zote.
Wakizungumza katika uwanja wa Sokoni, baadhi ya wamiliki wa viwanja ambao watatakiwa kulipa fidia walisema wamekubali na hawawezi kupingana na serikali.
“Hatupingani na serikali na tunaamini tutapata na kulipa kidogokidogo “alisema Omar Mgaza
Wakili Hamis Mkindi wa kituo cha sheria na haki za binaadamu(LHRC) ambao wamekuwa wakimtetea bibi huyo, amesema wanaridhishwa na hatua ambazo zinaendelea kuhakikisha bibi Muruo anapata haki.
Waziri Lukuvi Agosti 8,2019 akizungumza na pande zote katika mgogoro huo, alisema baada ya kazi ya upimaji viwanja katika kaya109 kukamilika, itafanyika tathimini ya kila kaya kumlipa kiasi gani bibi huyo na ambao watashindwa kwa muda utakaowekwa makazi yao yataondolewa na eneo hilo kukabidhiwa bibi huyo.
Hata hivyo, Waziri Lukuvi aliagiza eneo la wazi katika ekari hizo nane, akabidhiwe bibi huyo baada ya kulipima.
Tags: MIGOGORO YA ARDHIWILLIAM LUKUVI
ADVERTISEMENT
I am Magnifico

I am Magnifico

Related Posts

Mvua zaleta Majanga Mtwara
HABARI TANZANIA

Mvua zaleta Majanga Mtwara

by Ombeni Osward
Jan 14, 2021
0

Mvua zinazoendele Mtwara zimesababisha watu kukosa makazi...

Read more
ACT Wazalendo yajipanga kutetea Wanufaika wa mikopo ya Elimu ya juu

ACT Wazalendo yajipanga kutetea Wanufaika wa mikopo ya Elimu ya juu

Jan 14, 2021
Waziri ampa siku 7 IGP kushughulikia bajeti ya Mbwa

Waziri ampa siku 7 IGP kushughulikia bajeti ya Mbwa

Jan 11, 2021
Wahitimu Chuo Cha Maji Wanaajirika – Aweso

Wahitimu Chuo Cha Maji Wanaajirika – Aweso

Jan 9, 2021
Dk Ali Mohamed Shein Asimikwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe

Dk Ali Mohamed Shein Asimikwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe

Jan 5, 2021
General wa Jeshi aliemfurumusha Idd Amin Dada Atimiza miaka 101

General wa Jeshi aliemfurumusha Idd Amin Dada Atimiza miaka 101

Jan 4, 2021
Next Post
Chuo Kikuu UDSM Chakanusha Matokeo Mabaya Kwa Wanafunzi Wake

Chuo Kikuu UDSM Chakanusha Matokeo Mabaya Kwa Wanafunzi Wake

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

August 2019
M T W T F S S
« Jul   Sep »
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
262728293031  
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In