Mwanaharakati Mzalendo

BILLIAT AZIDI KUWACHANGANYA KAIZER CHIEFS NA MAMELODI SUNDOWNS

Nchini Afrika Kusini kumekuwa na mshtuko mkubwa juu ya sakata la mchezaji fundi Khama Billiat ambaye pia ni nyota wa Zimbabwe na Kaizer Chiefs kujiunga na Mamelodi Sundowns ya nchini humo. 
 
Wakati michuano ya AFCON 2019 inaendelea Sundowns waliwasiliana na viongozi wa Chiefs juu ya uhamisho wa nyota huyo lakini chini ya mwenyekiti Kaizer Moutang, Chiefs waligomea dili hilo. 
Utata unakuja hapa, baada ya viongozi wa Chiefs ‘kuchomoa’, inaaminika Sundowns wakaendelea na mbinu za chini chini ili kuinasa saini ya Billiat.
Kupitia vyombo vya habari vya nchi hiyo, kiongozi wa Sundowns alinukuliwa akisema wanamalizana na Billiat na atakuwa mchezaji wao rasmi siku za karibuni.
Chiefs wamegeuka mbogo juu ya taarifa hiyo na wamesema wataishitaki klabu hiyo kwenye mamlaka za michezo.
Namna gani tena wajukuu wa Mandela, au ndio matajiri hao wawili wanaonyeshana ubabe?, ikumbukwe Sundowns inamilikiwa na ‘tycoon’ Patrick Motsepe, huku ndoto yake ikiwa ni kumuona Billiat ndani ya dimba la Lucas Masterpiece Maripe!.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *