Chuo Kikuu cha Dar es Dalaam (UDSM) chakanusha uvumi unaonendelea kwenye mitandao ya kijamii kuwa wanafunzi wengi wamefeli mitihani ya chuo hicho.
Ni siku chache baada ya matokeo ya chuo hicho kutoka taarifa zilisambaa mitandaoni ikieleza kuwa wanafunzi wengi zaidi ya 1000 wamedisco yaani kutoendelea na masomo yao kabisa na wengine kurudia mitihani (supplementary)
Kupitia barua ilioyotolewa na chuo hicho, kimesema kuwa hizo taarifa sio za kweli kwani chuo kina utaratibu wa Kusimamia utungaji wa mitihani, usimamizi, ufanyaji na usahihishaji wa Mitihani
Barua hiyo inaeleza kuwa SENETI ndio linatoa maamuzi ya mwisho ya matokeo na Seneti haijafanya kikao chochote za kufanya maamuzi hayo.
Mwisho chuo kinawasihi na kuwatoa wasiwasi wanafunzi wa chuo hicho, wazazi, wanajumuiya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na wanajamii kwa ujumla kuwa taarifa hizo ni uzushi.
Pia kinawakumbusha wadau, wanafunzi na wafanyakazi kuwa chuo kina wajibu wa kusimamia ubunifu, utendaji kazi na maadili yao.
![]() |
Barua kwa umma |