Mwanaharakati Mzalendo

MUHUDUMU AUAWA KWA KUCHELEWESHA CHAKULA PARIS, UFARANSA

Mhudumu mmoja wa mgahawa jijini Paris amepigwa risasi hadi kufa na mteja ambaye amedaiwa kwamba alikuwa amekasirishwa kwa kuwa sandwich yake haikuandaliwa haraka iwezekanavyo.
Maafisa wa polisi wanasema kwamba uchunguzi umeanzishwa baada ya tukio hilo siku ya Ijumaa jioni mashariki mwa eneo la Le-Grand ambapo Mshukiwa alitoroka katika eneo hilo na hajapatikana mpaka wakati huu.
Wafanyakazi wa ambulensi walijaribu kuokoa maisha ya mhudumu huyo ambaye alikuwa amepigwa risasi katika bega lake lakini alifariki papo hapo.
Wenzake waliwaambia maafisa wa polisi kwamba mteja huyo alikuwa na hasira katika duka hilo la Pizza na Sandwich kutokana na muda mrefu ambao sandwich hiyo ilichukua kuandaliwa.
Mauaji hayo yamewashangaza wakazi wengi na wamiliki wa maduka.
“Inasikitisha”, mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 29 aliambia chombo kimoja cha habari nchini Ufaransa.
“Ni mgahawa uliotulia sana na hauna matatizo. Ulifunguliwa miezi kadhaa iliyopita.”
Baadhi ya wakazi hatahivyo wamesema kwamba kumekuwa na ongezeko la visa vya uhalifu katika eneo hilo mbali na ongezeko la visa vya ulanguzi wa mihadarati pamoja na unywaji pombe barabarani.  

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *