Basi la Kampuni ya Abood Bus Service ambalo linafanya safari zake kati ya Dar es salaam kwenda Mwanza limepata ajali mapema leo asubuhi maeneo ya Mkolani jijini Mwanza.
Inadaiwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendesha pikipiki kuingia barabarani bila ya tahadhari hivyo kusababisha dereva wa basi kupoteza mwelekeo.
Katika ajali hiyo taarifa za awali zinasema kuna kifo cha mtu mmoja ambaye ni dereva wa pikipiki huku watu kadhaa wakijeruhiwa.