Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) anayeshughulikia elimu, Ndg. Tixon Nzunda juzi Jijini Mwanza, Wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha kuandaa vipindi vya redio kupitia Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (MKUE-Tanzania).
Akieleza sababu ya marufuku hiyo, Ndg. Nzunda amesema kuwa vitendo hivyo vinasababisha wanafunzi wa madarasa hayo kuogopa na kutokuwa wasikivu wakati wa masomo.
Kwa mujibu wa sheria ya Elimu, Sura ya 353, Kanuni ya 3(1), marejeo ya mwaka 2002, imeeleza kuwa adhabu ya viboko itatolewa iwapo patatokea utovu mkubwa wa nidhabu au kosa kubwa litakalofanywa ndani au nje ya shule.
Kwenye sheria hiyo, Katika kanuni ndogo ya (2) inasema adhabu ya viboko itolewe kwa kuzingatia umri, jinsia na afya ya mwanafunzi na isizidi viboko vinne kwa tukio lolote.
Kwa upande mwingine, Nzunda ametoa wito kwa wadau wa elimu kushirikiana na Serikali katika kujenga mazingira mazuri ya utoaji elimu nchini ikiwemo ujenzi wa madarasa, vyoo na nyumba za walimu.