Mwanaharakati Mzalendo

Tetesi na Habari Za Soka Barani Ulaya leo 26/08/2019

Mabingwa watetezi PSG waibuka na ushindi wa 4-0 dhidi ya Toulouse hapo jana lakini habari inayowasumbua kichwa mashabiki wa timu hiyo ni kuwa Kinda Kylian Mbappe pamoja na Mshambuliaji Edison Cavani wametolewa nje wakiwa majeruhi. 

Mshambuliaji wa SS Lazio, Ciro Immobile amefikisha magoli 101 katika ligi kuu ya Italia maarufu kama Serie A. 


Beki Gerald Pique hapo jana dhidi ya Real Betis alicheza mechi yake ya 500 akiwa na FC Barcelona. 


Mshambuliaji Sergio Kun Aguero hapo jana alifikisha magoli 235 akiwa na klabu yake ya Manchester City katika mechi dhidi ya Bournemouth na magoli 400 katika maisha yake ya soka la kulipwa. 


Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane (Zizzou) amewaomba mashabiki wa timu hiyo waendeleze mshikamano baada ya droo ya 1-1 hapo juzi dhidi ya Real Valladolid pale Santiago Bernabeu. Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *