Mwanaharakati Mzalendo

Tetesi na Habari Za Soka Barani Ulaya Leo 27/08/2019

Mshambuliaji Mauro Icardi amesema kuwa hataki timu yoyote zaidi ya Inter Milan. Na katika kujazia hilo, Wakala wake ambaye pia ni mke wake aitwaye Wanda Icardi amesema “Kuna ofa nyingi zimekuja ambazo sidhani kama kuna mchezaji duniani angezikataa… Lakini Mauro Icardi amezikataa zote kwa ajili ya Inter”.

Mshambuliaji wa klabu ya PSG, kinda Kylian Mbappe anaaminika atakaa nje kwa takribani wiki 3 hadi 4 kutokana na jeraha la paja alilolipata hapo jana katika mchezo dhidi ya Toulouse. 
Kinda wa Atletico Madrid Joao Felix amezidi kupokea baraka toka kwa wachezaji wenzake wa klabu hiyo na kwa sasa ni golikipa wao Jan Oblak. “Nilikuwa najua wazi kuwa Joao ana uwezo mkubwa Sana… Naamini atakuja kuwa mmoja wa wachezaji wakubwa sana duniani”


Jerzy Dudek huyu ni golikipa wa zamani wa klabu ya Liverpoool akiongea kuhusu mtu anayeweza kuchukua mikoba ya Jurgen Klopp pale Anfield alisema “Steven Gerrard ndio mtu sahihi anayaweza kuchukua nafasi ya yule mjerumani pale Anfield, Kila mtu anajua muda si mrefu nahodha mkuu anaweza kurejea.” 


Romelu Lukaku ameanza vyema maisha yake ndani ya klabu yake mpya ya Intermilan baada ya hapo jana kucheza mechi yake ya kwanza na kufunga goli dakika ya 60. Goli hilo lilikuwa ni la 3 katika ushindi wa 4-0 walioupata Inter dhidi ya LECCE. 


Klabu ya Tottenham inahofia huenda kiungo wake Christian Eriksen anaweza kuondoka klabuni hapo kutokana na thamani yake kushuka hadi pauni Milioni 30. Mkataba wa Eriksen na Tottenham unafika tamati mwishoni mwa msimu huu na klabu za Atletico Madrid na Real Madrid zinaripotiwa kuitaka saini yake. Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *