Mwanaharakati Mzalendo

Tetesi na Habari za soka Barani Ulaya leo 28/08/2019

Inter Milan wamefikia makubaliano ya kumsajili Alexis Sanchez kutoka Manchester United kwa mkopo na kesho nyota huyo wa Chile anatarajiwa kutua Jijini Milan (Italia) kwa ajili ya vipimo vya afya. [Sky Sports Italy]
Mkurugenzi mkuu wa klabu ya Inter Milan, Beppe Marotta anapinga vikali maneno ya mke na wakala wa Mauro Icardi kuwa klabu ya Inter kupitia Rais wake wamemuomba Mauro Icardi abaki klabuni hapo. 


 Mshambuliaji Emmanuel Adebayor amejiunga na klabu ya Kayserispor kwa mkataba wa mwaka mmoja. Adebayor ameshachezea klabu kama AS Mpnaco, Arsenal, Real Madrid, Tottenham Hotspur, Crystal Palace, FC Metz na nyinginezo. 


Klabu ya FC Barcelona yafungua uwanja mpya kwa heshima ya gwiji wa klabu hiyo Johan Cruyff. Uwanja huo umepewa jina la Johan Cruyff kwa heshima ya mchango mkubwa aliouleta katika klabu hiyo. Familia ya Cruyff ikiongozwa na mkewe Danny pamoja na watoto wake wawili Jordi na Susila walikuwa wageni rasmi wa shughuli hiyo ya ufunguzi. Uwanja huo utakuwa mahususi kwa ajili ya michezo ya Barca B na Timu ya wanawake ya Barcelona.


Kocha mpya wa Inter Milan, Antonio Conte, anaamini kuwa mshambuliaji wake mpya Romelo Lukaku ndio kwanza anaanza kuonesha uwezo wake katika soka na anaamini anaweza kuwa mmoja wa wachezaji wakubwa sana duniani. 


Baada ya Mo Salah kuiponda VAR, sasa ni zamu ya Kiungo wa Man City Ikay Gundogan. Yeye amesema “VAR inabadilisha mpira sio tu kwa wachezaji bali pia mashabiki na kila mmoja anayependa mpira. Kwa bahati mbaya inaondoa sababu kuu ya kwanini tunapenda soka” [Skysport]


PSG Wapo tayari kuwauzia Barcelona mchezaji Neymar kwa gharama ya Euro Milioni 100 huku wakijumuishwa na wachezaji Ousmane Dembele pamoja na Nelson Semedo [Le Parisien] Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *