Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Liverpool FC, Muingereza Daniel Sturridge amejiunga na Klabu ya trabzon spor ya Uturuki kama mchezaji huru.
Klabu ya AS ROMA yathibitisha kumnasa beki Davide Zappacosta kwa mkopo kutokea klabu yake ya Chelsea FC.
Sissoko Moussa, ambaye ni Meneja wa Mchezaji na winga wa FC Barcelona Ousmane Dembele amesema kuwa mchezaji huyo hatishwi na ujio wa Neymar katika klabu hiyo kwani Dembele anajua kuwa kucheza katika klabu kama Barcelona huwezi kukwepa ushindani.
Thiery Henry bado anaamini kuwa atakuja kuwa kocha mkubwa na mzuri sana hapo baadaye. Ameyasema hayo akiwa anahijiwa na The Telegraph
Baada ya kuumia na kukosa mchezo wa kwanza wa msimu, Mshambuliaji wa FC Barcelona Lionel Messi amerudi mazoezini na wachezaji wenzie wa FC Barcelona na kuna uwezekano mkubwa akawepo katika kikosi kitakachocheza mechi ya mzunguko wa pili wa Ligi kuu ya Hispania maarufu kama LALIGA wikiendi hii.
Inter Milan na Manchester United wapo katika hatua za mwisho kabisa za kukamilisha uhamisho wa winga Alexis Sanchez kwa mkopo na ishu ya mshahara ndio inayosumbua mazungumzo hayo.
Aliyekuwa Winga wa klabu ya FC Bayern Munich na Timu ya taifa ya Ufaransa, Frank Ribery, 36, amejiunga na klabu ya Fiorentina ya Italia akiwa mchezaji huru.
Cristiano Ronaldo akihojiwa na kituo cha TV1 cha kwao Ureno ametaja tuhuma za ubakaji ziilimfanya aone mwaka 2018 ndio mwaka mbaya katika maisha yake.