City wamekataa dau la pauni milioni 72 kutoka kwa Bayern Munich kwa
ajili ya mshambuliaji wa Leroy Sane raia wa Ujerumani, mwenye umri wa
miaka 23. (Metro)
![]() |
City wanataka walipwe pauni milioni 137 kwa
mauzo ya Sane ikiwa hatakuwa na haja ya kusaini mkataba wa kurefusha
mkataba wake, unaomalizika Juni 2021. (Telegraph)
Manchester
United wanahangaika kufikia makubaliano na mshambuliaji wa Argentina
Paulo Dybala, mwenye umri wa miaka 25, na muwakilishi wake, na hivyo
kuuweka hatarini mkataba na Juventus wa kubadilishana mchezaji wa safu
ya mashambulizi Mbelgiji Romelu Lukaku, mwenye umri wa miaka 26.
(Independent)
Manchester City imeingia tena katika mazungumzo na
Juventus juu ya kiungo wa safu ya nyuma kulia Mremo Joao Cancelo,mwenye
umri wa miaka 25. (Telegraph)
Mlizi wa England Harry Maguire,
mwenye umri wa miaka 26, ameachwa nje ya kikosi cha Leicester
kitakachocheza mechi ya urafiki baina yao na Atalanta Ijumaa kutokana na
hali ya sintohfahamu juu ya hali ya yake ya baadae na Foxes wanaotaka
mkataba wa pauni milioni 90 ikiwa Manchester United wanasaini mkataba
nae. (Telegraph)
Dau la sasa la Manchester United kwa ajili ya
Maguire ni la thamani ya pauni milioni 80 na klabu hiyo inaweza kutumia
zaidi ya pauni milioni 150 kwa ujumla kabla ya kipindi cha mwisho cha
mchakato wa uhamisho kukamilika (Independent)
Manchester United
ilikataa fursa ya kusaini mkataba na mshambuliaji wa Juventus mwenye
umri wa miaka 19 Moise Kean, na kumruhusu mtaliano huyo kuwa huru
kuhamia Everton. (90min)
Liverpool wanapima uwezekano wa kumnunua
mchezaji wa safu ya mashambulizi wa Bordeaux na Guinea Francois Kamano
na wako tayari kumgaramia kwa pauni milioni 20 kijana huyo mwenye umri
wa miaka 23 . (Sun)
Tottenham wanauangalia mkataba kwa ajili ya
kiungo wa kati wa Sporting Lisbon na Ureno Bruno Fernandes, mwenye umri
wa miaka 24, kama kiungo mbadala wa mchezaji wa Real Beti -Giovani Lo
Celso, mwneye umri wa miaka 23. (Evening Standard)
Betis
wamekataa ofa kadhaa kutoka kwa Tottenham kwa ajili ya mchezaji wa
kimataifa wa Argentina Lo Celso. (SevillaABC – in Spanish)
Kiungo
wa kati- nyuma wa Argentina Nicolas Otamendi, mwenye umri wa miaka 31,
anataka kuendelea kuwepo Manchester City licha ya kuhusishwa na taarifa
za kuihama klabu hiyo.(Sun)
Newcastle wanakaribia kusaini mkataba
na winga wa Ufaransa Allan Saint-Maximin,mwenye umri wa miaka 22,
kutoka Nice katika mkataba wa pauni milioni 16.5 . (Talksport)
Mchezaji
wa safu ya nyuma-kushoto wa Brazil Dani Alves anakaribia kuhamia Sao
Paulo. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 36- yuko huru baada ya kuondoka
Paris St-Germain. (Goal)
Crystal Palace wamefany amawasiliano na
Cardiff City kumuhusu kiungo wa kati wa Real Betis Muhispania Victor
Camarasa mwenye umri wa miaka 25