Mwanaharakati Mzalendo

WASHINDI WA PROMOSHENI YA ‘AMSHA NDOTO’ WATANGAZWA NA BENKI YA AZANIA

Benki ya Azania (ABL) leo imewatangaza washindi wa promosheni yake ya ‘Amsha Ndoto’ ambayo ina lengo la kuwahamasisha wateja wake na umma wa watanzania kujenga utamaduni wa kuweka akiba itakayowasaidia kuwa na maisha ya baadaye yaliyo imara kifedha. 
Meneja wa Mauzo ya Reja Reja wa Benki ya Azania
Meneja wa Mauzo ya Reja Reja wa Benki ya Azania, Jackson Lohay (katikati) akiongea kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa promosheni ya ‘Amsha Ndoto’ katika droo iliyofanyika katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam. Jumla ya Sh. 8,000,000/- ilitolewa kwa washindi watatu walioshiriki katika promosheni hiyo.
Promosheni hii ambayo ni ya mizezi mitatu ilianza rasmi tarehe 27/06/2019 na inatarajia kufikia tamati tarehe 27/09/2019 huku ikihusisha wateja wa Azania Benki wa zamani na wale wapya na imejikita zaidi katika bidhaa mbili kuu za uwekaji akiba, ambazo ni: Ziada Akaunti pamoja na Watoto Akaunti. 
Akitangaza washindi kwenye droo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, Meneja wa Mauzo ya Reja Reja wa Benki ya Azania, Jackson Lohay, amesema benki imetimiza ahadi ya kuwapatia zawadi washindi walioshoriki kwenye promosheni na kwamba zawadi wanazopewa zitawasaidia kutimiza ndoto zao. 
Kwa mujibu wa Lohay, washindi wa mwezi Julai wa promosheni hii ambao wamepatikana baada ya droo kufanyika ni; 
1. Barakaeli Mmari amejishindia kiasi cha TZS 2,000,000/- (Arusha) 
2. Rose Anaeli amejishindia kiasi cha TZS 3,000,000/- (Dar es Salaam) 
3. Ketus Isack Malekamo amejishindia kiasi cha TZS 3,000,000/- (Tunduma) 
Lohay ameongeza kuwa ili mtu aweze kushiriki kwenye promosheni ya Amsha Ndoto ni lazima kwanza awe mteja wa Azania Benki mwenye akiba ya kiasi kisichopungua TZS 1,000,000 ambaye anapewa tokeni zinazomwezesha kufuzu kwa ajili ya droo ya mwisho inayowapata washindi. Wanaobahatika kushinda watafurahia riba ya 6% katika kipindi chote cha kampeni na mwaka mzima. 
Akitoa pongezi kwa washindi wa promosheni, Lohay amewahasa wateja wa ABL kushiriki kwa wingi na kwamba wana nafasi kubwa ya kujishindia zawadi lukuki katika droo zinazofuata huku wakijahakikishia kuwa na akiba ya kutosha kwenye akaunti zao kwa ajili ya matumizi yao ya siku za usoni. 
“Tunawahamasisha wazazi wote na walezi kuwafungulia Watoto wao ‘Watoto Akaunti’ ili kuwa na uhakika wa maisha yao ya baadaye yaliyo salama. Kwa namna hii hawatahangaika kutafuta namna gani ya kuwaandaa watoto wao kwa maisha ya baadaye kwani akaunti hii inaweka msingi wa kuwaandaa watoto kujifunza namna ya kuweka akiba kuanzia kwenye umri mdogo”, amesema Lohay. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *