Mwanaharakati Mzalendo

ZANZIBAR: WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUWABAKA NA KUWADHALILISHA WATOTO WA MIAKA 12

Akisomewa shtaka lake na mwendesha mashtaka wa Mahakama hiyo, Ali Amour Makame, mtuhumiwa huyo alikana kutenda kosa hilo na kuiomba mahakama impe dhamana.
“Mheshimiwa hakimu, mimi sijafanya jambo hilo wananisingizia tu, naiomba mahakama yako inipatie dhamana,” alidai mtuhumiwa huyo.
Hakimu Abdalla Yahya Shamhuna, alikubali ombi la dhamana aliloomba mshtakiwa na kusema kesi hiyo itarudi tena mahakamani Agosti 19, mwaka huu.
Ilidaiwa mahakama hapo mtuhumiwa alitenda kosa hilo siku na tarehe isiyofahamika Jauari mwaka 2018 saa 7:00 mchana Mkanjuni Mtambwe Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Ilidaiwa kuwa, bila ya halali alimbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 12.
Kufanya hivyo ni kosa kisheria kinyume cha kifungu cha 125 (1) (2) (e) na kifungu cha 126 (1) cha Sheria namba 6 ya mwaka 2004, Sheria ya Zanzibar.
Wakati huo huo, mahakama hiyo imempandisha kizimbani Juma Hamad Hassan (75) mkaazi wa Mkanjuni Mtambwe Kusini kwa tuhuma za kumfanyia unyanyasaji mkubwa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 12.
Akisomewa shtaka lake na mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo, Ali Amour Makame, mtuhumiwa alikana kutenda kosa hilo na kuiomba mahakama impe dhamana.
Hakimu wa mahakama hiyo, Abdalla Yahya Shamhuna, alikubali ombi la dhamana aliloomba mshtakiwa na kusema atakapokamilisha masharti yaliyotakiwa mahakama itampatia dhamana.
“Mtuhumiwa dhamana zako ziko wazi na utapewa dhamana utakapokamilisha masharti yaliyotakiwa,” alisema hakimu.
Mtuhumiwa aliyakamilisha masharti ya dhamana na kesi hiyo itarudi tena mahakamani Agosti 19, mwaka huu.
Ilidaiwa mahakama hapo kuwa, mtuhumiwa alitenda kosa hilo Julai 11, mwaka jana, mchana, Mkanjuni Mtambwe Kusini Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Ilidaiwa bila ya halali na kwa ajili ya kukidhi matamanio yake ya kimwili, alimvua nguo mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 12 na kumfanyia udhalilishaji.
Kufanya hivyo ni kosa kisheria kinyume cha kifungu cha 139 (1) (a) na (2) (a) cha sheria namba 6 ya mwaka 2018 Sheria ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Chanzo: Nipashe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *