Mwanaharakati Mzalendo

Benki zimeshusha riba za mikopo, vyuma havikazi tena”_ Dk Mpango:


Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema kutokana na juhudi za taasisi za fedha kushusha riba za mikopo zinazotoa kwa wateja wao, sasa hivi hasikii tena watu wakisema vyuma vimekaza.

Dar es Salaam. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema kutokana na juhudi za taasisi za fedha kushusha riba za mikopo zinazotoa kwa wateja wao, sasa hivi hasikii tena watu wakisema vyuma vimekaza.
Mpango amesema hayo leo Alhamisi Septemba 19, 2019 wakati akizindua kanuni za utendaji za huduma za benki zilizoandaliwa na Chama cha Wakuu wa Benki Tanzania (TBA).
“Nazipongeza benki zote za biashara kwa kushusha riba na BoT (Benki Kuu ya Tanzania) kuongeza ukwasi. Sasa hivi sisikii tena watu wakisema vyuma vimekaza,” amesema Dk Mpango.
Hata hivyo, waziri huyo amezitaka taasisi ndogo za fedha kufuata mkondo huo kwani riba zinazotoza bado ni kubwa na zinawaumiza wananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *