Mwanaharakati Mzalendo

Achana Na Albamu, Filamu Fupi Ya ‘JESUS IS KING’ Ya Kanye Yatikisa Dunia

Tukujuze tu kwamba Kanye West hakuachia album ya “Jesus Is King” pekee, fahamu pia aliachia na filamu fupi yenye jina hilo hilo.
Filamu hiyo yenye dakika 30 ni mkusanyiko wa matukio ya nyuma ya pazia kwenye ibada zake za Jumapili, ikiwa na siku moja sokoni tayari imetengeneza kiasi cha ($1.03M) katika Box Office ndani ya Wikendi ya ufunguzi.
Kwa mujibu wa Variety, filamu hiyo imekusanya jumla ya bilioni 1.9 za Kitanzania katika majumba 372 ya IMAX Marekani na pia zaidi ya milioni 400 za Kitanzania katika majumba 68 ya filamu katika masoko 12 ya Kimataifa. IMAX pia imepanga kuongeza mataifa 78 November 8 mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *