Mwanaharakati Mzalendo

Alikiba amjibu Diamond kwa ghadhabu kisa mwaliko wa Wasafi Festival “Nikuweke uchi watu wajue unayonifanyia?”

Baada ya msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kutangaza kuwa Meneja wake, Babu Tale ameshafanya mawasiliano na Alikiba kuhusu ushiriki wake wa kwenye tamasha la Wasafi Festival, Hatimaye Alikiba amemjibu Diamond tena kwa ghadhabu.

Diamond na Alikiba

Alikiba ametumia ukurasa wake wa Instagram kumjibu Diamond kwa kuandika, Usiniletee mambo ya darasa la Pili unaniiibia penseli alafu unanisaidia kutafuta .(UNIKOME) Mwanaume huwa anaongeaga mara moja tu sasa ukitaka nikuweke uchi watu wajue unayonifanyia hata kwenye hilo tamasha hatokuja mtu sasa tuishie hapo nakutakia tamasha njema @diamondplatnumz,“.
Hii ni mara ya pili kwa Alikiba kukataa kutumbuiza kwenye tamasha hilo la Wasafi Festival, Alifanya hivyo pia mwaka jana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *