Mwanaharakati Mzalendo

KHALIGRAPH JONES Achapiwa Cheni Yake Ya Gharama Akitumbuiza Kisumu

Khaligraph Jones alirudi nyumbani shingo upande baada ya kuvuliwa cheni yake ya gharama wikendi hii wakati akitumbuiza kwenye party ya Guinness Smooth launch Party Jumamosi mjini Kisumu.

Papa Jones alikuwa miongoni kwa watumbuizaji wa party hiyo akiwemo pia Sailors, Willy Paul. Baada ya stage kukolea, Khaligraph alishuka Stejini na kuwafata mashabiki ambapo haikuchukua muda shabiki mmoja alimvua cheni yenye thamani ya (Kshs. 60,000) sawa na milioni 1.3 za Kitanzania.
Khaligraph alitangaza kwamba “Wameenda mpaka na chain, but ni sawa sisi tunapeana kila kitu. Kisumu nawapenda bado juu hata hii show niliambia organizers nitapiga free. So mjue hivyo ndio nawapenda.” Alisema Khaligraph baada ya kurudi stejini.
“Hiyo chain wameenda nayo ilikuwa 60K but hizo ni vitu ndogo Mimi nilikuja kuua show.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *