BASHE Awasha Moto, Amsimamisha kazi Kigogo mmoja na kutaka Bil 4.5 Zirudishwe Haraka

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema Serikali imemsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC), pamoja na kumuagiza Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya BAJUTA kuzirudisha haraka iwezekanavyo, fedha za umma kiasi cha Tsh.Bilioni 4.5.
“Ni kweli Serikali ilitoa pesa Bilioni 10 kwa ajili ya kuagiza viuatilifu hivyo na Serikali imemsimamisha Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya TFC kama hatua ya awali kwa uzembe huu”- BASHE
“Nitumie nafasi hii kumtaka Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya BAJUTA kurudisha Bilioni 4.5 alizopewa na tumeongea na TPA wamekubali kutuondolea gharama zote na sasa tuko katia hatua za mwisho kuvitoa viuatilifu hivyo kabla havijaharibika ili tuwagawie wakulima” -BASHE

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *