Mwanaharakati Mzalendo

Ben Pol ataja Wanamuziki 15 anaowaona ni bora

Msanii wa muziki wa kizazi kipya na mwigizaji nchini Benard Paul maarufu kama Ben Pol,  ametoa orodha ya Wasanii 15 wa muziki ambao kwake anaamini ni bora katika kipindi cha miaka  Ishirini.

Ben Pol ametoa orodha hiyo kupitia ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa twitter ambapo amemuweka Marehemu Albert Mangwea(Ngwair)katika nafasi ya kwanza.

Ben Pol anayeimba zaidi miondoko ya RnB, alianza kuvuma katika muziki mwaka 2010 baada ya kutoa kibao chake cha  Nikikupata,  ambacho kiliweza kumtambulisha vyema katika ulimwengu wa Bongo Flava.

Nyimbo nyingine za msanii huyo ni
Samboira, Moyo Mashine, Jikubali, Namba One Fan, Tatu na Sophia na nyinginezo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *