Mwanaharakati Mzalendo

KOCHA YANGA AIBUA SIRI YA KANDA KUSAINI SIMBA, ASEMA ALIKUWA NA MATATIZO ‘HAKUCHEZA’Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema kuwa mabosi wa Simba walimsajili winga kutoka TP Mazmbe, Deo Kanda kutokana na historia yake ya mpira.

Zahera ameeleza licha ya usajili huo kufanyika, Kanda alikuwa na matatizo ndani ya Mazembe kitu ambacho anaamini kilimpa urahisi kuondoka pale.

Zahera amefunguka kwamba Kanda alikuwa hapatai nafasi ndani ya kikosi cha TP Mazembe hivyo ikawa ni urahisi kwa Simba kupata saini yake.

“Soka la Afrika lina tatizo, unajua Simba nani alienda kumuona Deo Kanda akicheza?

Jibu hakuna, ila ukweli alikuwa na shida na timu yake TP Mazembe, hakuwa anacheza ligi lakini Simba wakamsajili.

“Huwezi sema Simba walikosea kwa kuwa Kanda ni mchezaji mzuri na wamemchukua kutokana na historia yake.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *