Mwanaharakati Mzalendo

KUMBE KAGERE ANATESWA NA REKODI YAKE YA MABAO BONGO


REKODI ya mabao 23 aliyoweka mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere imekuwa ikimpa taabu kutokana na ugumu wa ligi ulivyo kwa sasa ndani ya ligi pamoja na kufikiria namna ya kuipa mataji timu yake.

Kwa sasa Kagere ambaye ni raia wa Rwanda ametupia jumla ya mabao nane timu yake ikiwa imecheza jumla ya mechi 9 ikiwa na pointi 22 kibindoni.

“Ushindani ni mkubwa kwa sasa kila mchezaji ana malengo yake kwangu mimi lengo la kwanza ni kuipa mataji timu yangu kisha suala la ufungaji litafuata maana nikifikiria tuzo itakuwa haina maana kwangu.

“Kwa sasa tupo tayari kwa ajili ya ushindani na kufanya kazi kwa ajili ya kupata matokeo, tunajua mashabiki wanahitaji nini nasi tunahitaji nini waendelee kutupa sapoti,” amesema Kagere

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *