Mwanaharakati Mzalendo

Mbosso apewa onyo kuondoka WCB

Mkubwa Fella ambaye ni miongoni mwa Team Managers wa Diamond Platnumz amempa onyo msanii wa muziki kutoka kwenye lebo ya WCB.

Mkubwa Fella aliweka picha Mbosso katika ukurasa wake wa Instagram na kuandika; “Nasema mwanangu Mbosso piga kazi kumbukizi zisikulazimu kumuonea huruma utakaye kutana nae jukwaani pambania kumkalisha utakae muona ila tanguliza bendera yetu ya nchi yetu ya Tanzania pia uza brand yako WCB Wasafi.”

“Ila nakusihi unaenda kwenye ukubwa sasa wasijitokeze wanao kushawishi ujitoe kumbuka mkataba mwanangu, muda huu wanajifanya kama hawakuoni tunapambana sisi tu Kwenye ukuwaji wako Mkubwa Fella, diamond Platnumz, Babutale na Sallam ila baadae wanajitokeza wanao kuona biashara sasa Mwanangu wakija kukushawishi wakumbushe una mkataba.”


“Wakiweza waje wasije wakakurubuni baadae tukiwambia gharama za ukuaji wako wana kimbia badae wanakuacha baadae tuna wapa shida wakuu kwa kutojua undani kumbe umesakiziwa na wapenda vilivyo andaliwa ayaa wadau mwanetu mboso uyoooo umangani ila tarehe 9 atakuwepo Wasafi Festival19 Dar.”


Kwa upande wake Mbosso alimjibu Mkubwa Fella kuwa “Nimekuelewa vizuri Mkubwa.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *