Mwanaharakati Mzalendo

MKWASA AJA NA MBINU MBADALA ZA KUREJESHA FURAHA YANGA


Baada ya kukabidhiwa majukumu ndani ya kikosi cha yanga, Kaimu Kocha Mkuu, Boniface Mkwasa, amesema hivi anachokifanya ni kuwajenga kisaikolojia wachezaji wa timu yake. Imeelezwa.

Taarifa imesema Mkwasa amesema hayo baada ya kuwa na mwenendo mbaya ndani ya kikosi hicho hususan katika mechi za kimataifa pamoja na ligi.

Kauli ya Mkwasa imekuja kutokana na kuiongoza timu yake kupata matokeo katika mechi ya kwanza tangu apewe mikoba ya Mwinyi Zahera kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda FC.

Mkwasa amedai kuwa wachezaji wengi wa Yanga walikuwa wamekata tamaa hivyo hivi sasa anajaribu kuwarejesha kwenye hali ya kawaida ili waweze kuendana na mipango yake.

Kocha huyo maarufu kama Master ameamua kufanya maamuzi hayo akiamini wachezaji wake hawakuwa vizuri kisaikolojia na hii itawasaidia kuwajenga vizuri zaidi siku za usoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *