Mwanaharakati Mzalendo

NEYMAR AKATAA OFA PSG BARCELONA MASHAKANI.

Neymar Akataa Mkataba mpya PSG , Barcelona Mashakani.

Nyota wa Paris Saint-Germain Neymar amekataa ofa ya kukabidhiwa mkataba mpya wa kuitumikia  PSG na kuonesha Kuwa na uwezekano wa kuhamia Barcelona.

Barcelona ilitumia mbinu za kushawishi PSG kumruhusu Neymar arudi Kamp Nou, lakini mbinu hizo ziligonga mwamba  kwa PSG kutoshawishika kumtoa Neymar.

Mabingwa hao  wa Ligue 1 wameonesha juhudi za kumbakishaba huko Paris, walianza kujadiliana mkataba mpya na Nyota Mbulazil msimu uliopita. Walakini, kulingana na Sport, Neymar hakuvutiwa kubaki.

Neymar Hana mpango wa kuongeza muda wake wa kukaa na PSG na angependa kurudi Barcelona kabla ya mkataba wake wa sasa kumalizika mnamo 2022.

Baba yake Neymar, ambaye anafanya mazungumzo kwa niaba ya mtoto wake, anasema kuwa anafanya maisha kuwa magumu kwa PSG, kwa matumaini ya kuwashawishi wamuuze.

Kama inavyosemekana Neymar anaweza kutaka kuondoka, lakini kuna vizuizi vingi sana katika usajiri wa Nyota huyo.

Je Barcelona watafanikiwa kumnyakua Neymar?. Licha ya kugomea mkatabaa mpya PSG.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *